Usimilisho wa Tenzi za Kale kama Njia ya Kukuza Uelewa wa Utamaduni na Historia kwa Watoto: Mfano wa Tenzi Za Fumo Liyongo na Mwana Kupona

https://doi.org/10.51317/eajk.v4i1.849

Authors

Keywords:

Fasihi ya watoto, historia, masimilisho, tenzi za kale, usimilisho, utamaduni

Abstract

Swahili

Tenzi za kale za Kiswahili ni hazina ya urithi wa historia na utamaduni wa Waswahili. Tenzi hizi zilitungiwa hadhira ya watu wazima. Aghalabu zimesheheni lugha ya kale, mitindo tata ya kishairi na maudhui ya kifalsafa na kidini. Hivyo, ni ngumu kwa watoto kuelewa tenzi za kale. Hali hii ni changamoto kwa watoto kupokea utamaduni na historia ya Waswahuli. Wasanii wa kisasa wamefanya jitihada kusimilisha  tenzi hizo kuwa fasihi ya watoto. Hata hivyo, tafiti hazijachunguza kwa kina usimilisho kama njia ya kuwasilisha utamaduni na historia. Makala hii imechunguza usimilisho wa tenzi za kale kama njia ya kukuza uelewa wa historia na utamaduni kwa watoto. Tenzi mbili; Fumo Liyongo na Mwana Kupona zilizingatiwa. Aidha, masimilisho ya tenzi teule; Kisa cha Fumo Liyongo (KcFL), Mkasa wa Shujaa Liyongo (MwSHL) na Wasifu wa Mwana Kupona (WwMK) yalitumika. Data ya utafiti ilikusanywa kupitia usomaji makini wa matini chaili na matini lengwa. Uchanganuzi wa data ulifanywa kwa misingi ya Nadharia ya Usimilisho ya Hutcheon (2013). Utafiti ulibaini kuwa historia ya mashujaa, mifumo ya kiutawala, dini, sherehe, vyakula na mavazi viliundwa upya kwa njia nyepesi na picha za kimaelezo ili kufaa hadhira ya watoto. Hivyo, usimilisho ulichangia katika kukuza ufahamu wa kitamaduni na kihistoria kwa vizazi vijavyo. Makala hii inapendekeza watafiti wa baadaye wachunguze kazi nyingine za usimilisho wa tenzi za kale kutoka tamaduni tofauti za Kiafrika.

English
Classical Swahili epics are a rich repository of the historical and cultural heritage of the Swahili people. These poems were originally composed for an adult audience. They are often characterised by archaic language, complex poetic styles, and philosophical as well as religious themes. As a result, they are difficult for children to understand. This poses a challenge for the transmission of Swahili culture and history to younger generations. Modern artists have made efforts to adapt these epics into children’s literature. However, few studies have examined adaptation as a means of transmitting culture and history. This paper examined the adaptation of classical Swahili epics as a way of enhancing children’s understanding of history and culture. Two epics, Fumo Liyongo and Mwana Kupona, were analysed along with their adaptations: Kisa cha Fumo Liyongo (KcFL), Mkasa wa Shujaa Liyongo (MwSHL) and Wasifu wa Mwana Kupona (WwMK). Data were collected through close reading of both source and target texts. The analysis was guided by Linda Hutcheon’s (2013) Theory of Adaptation. The study found that the depiction of heroes, systems of governance, religion, ceremonies, food, and clothing were creatively restructured in a simple and illustrative manner to suit a children’s audience. Therefore, adaptation contributed significantly to promoting cultural and historical awareness among younger generations. The paper recommends that future researchers explore other adaptations of classical African epics from different cultural contexts.

Keywords: Adaptation,  Classical Epics , Children’s Literature, Culture, History

Downloads

Download data is not yet available.

Published

2025-10-14

How to Cite

Mitambo, E. M., Musyimi , D. M., & Mugambi , A. (2025). Usimilisho wa Tenzi za Kale kama Njia ya Kukuza Uelewa wa Utamaduni na Historia kwa Watoto: Mfano wa Tenzi Za Fumo Liyongo na Mwana Kupona. Eastern Africa Journal of Kiswahili (EAJK), 4(1), 76–88. https://doi.org/10.51317/eajk.v4i1.849

Issue

Section

Articles

Similar Articles

1 2 > >> 

You may also start an advanced similarity search for this article.