Ukombozi wa mwanamke kiuchumi katika tamthilia za Kigogo na Chema Chajiuza

https://doi.org/10.51317/eajk.v4i1.80

Authors

Keywords:

kiuchumi, mwanamke, mwanamume, ukombozi, usawa

Abstract

SWAHILI

Utafiti huu umejihusisha na jinsi wanawake wanavyojikomboa kiuchumi katika tamthilia za Kigogo na Chema Chajiuza. Utafiti huu umeongozwa na nadharia ya Ufeministi wa Kiafrika iliyoasisiwa na Steady. Akiangazia masuala yanayohusiana na Ufeministi wa Kiafrika. Ufeministi huu hujihusisha na masuala ya wanawake wa Kiafrika kwa kuegemea utamaduni na mapana yake. Ufeministi wa Kiafrika hung’ang’ania kujijenga upya, mawazo huria ya wanawake na kujitegemea wenyewe katika asili zao mbalimbali za kitamaduni. Mihimili ya nadharia hii ni kielelezo katika kumpa mwanamke wa Kiafrika hadhi inayomstahiki kwa kuweka mikakati inayolingana na shida zinazomkabili katika mazingira yake. Kupitia nadharia hii, suala la jinsi wanawake wanavyojikwamua kiuchumi liliangaziwa. Makala husika yalitokana na usomi wa kina. Data iliyopatika kuwa muhimu ilichanganuliwa kupitia njia ya kimaelezo. Data husika ilikusanywa moja kwa moja kutoka maktaba na mtandaoni. Maktaba lengwa ni zile za vyuo vikuu na umma. Matokeo ya utafiti huu ni mwongozo bora kwa jamii nzima hasa wanawake ambao ndio kundi lengwa kujua hatua za kiuchumi wanazochukua wenzao ili kujiweka katika mizani sawa na wanaume.

Downloads

Download data is not yet available.

Published

2022-07-30

How to Cite

Kamau, P. M., & Wandera-Simwa, P. S. (2022). Ukombozi wa mwanamke kiuchumi katika tamthilia za Kigogo na Chema Chajiuza . Eastern Africa Journal of Kiswahili (EAJK), 1(1), 26–32. https://doi.org/10.51317/eajk.v4i1.80

Issue

Section

Articles