Uchunguzi wa Kiplato Kuhusu Udhibiti wa Maadili Katika Miziki Miwili ya Kisasa Nchini Kenya (Seti na Stick)
Abstract
Swahili
Utafiti huu ulichunguza umuhimu wa maoni ya mwanafalsafa Plato kuhusu fasihi. Nafasi ya maoni yake katika kudhibiti maadili kwenye miziki miwili katika nchi ya Kenya kwa ajili ya utovu wa maadili iliangaziwa. Miziki hii ni: Seti wa Bahati na Stick wa Khaligraph Jones. Licha ya mkazo uliowekwa kitamaduni na kidini katika nchi ya Kenya kuhusiana na maadili, kungali kuna miziki ya kisasa inayokweza utovu wa maadili. Miziki hii iliibua mihemko na chachawizo kutoka kwa watu wengi kwa ajili ya maudhui yaliyopo, walakini kudhibitiwa kwayo na serikali kungali kuna utata. Madhumuni ya utafiti yalikuwa kutathmini ikiwa miziki hii ilifaa kudhibitiwa kwa kupigwa marufuku kwa ajili ya kukiuka maadili katika maudhui yake kwa kutumia msimamo wa Plato kuhusiana na dhima za fasihi na kubaini mbinu za kimtindo kwenye miziki hii. Nadharia ya Sanaa ya Kimaadili ya Plato ilitumika kwenye utafiti huku mihimili yake ikihusishwa miongoni mwa madhumuni. Utafiti huu ni wa kithamano na ulitumia muundo wa kimaelezo kuchanganua na kuiwasilisha data. Data ilipakuliwa kwenye mtandao wa YouTube kisha picha na maneno kwenye miziki hii yakachanganuliwa. Usampulishaji ulikuwa wa kimakusudi kwa kuteua miziki miwili iliyokuwa imeibua malalamiko mengi kutoka kwa umma. Matokeo ya utafiti huu yanabaini kuwa miziki hii inasisimua hisia za kingono, ina uchafu mwingi, husababisha utovu wa maadili na kufisidi akili za hadhira kwa njia ambayo Plato angepinga. Hivyo, inasababisha mijadala ya udhibiti wa maudhui ya miziki hii ya kisasa nchini Kenya. Ilibainika pia kuwa miziki hii imetumia anaphora, kuhamisha ndimi, jazanda, udamisi, usafidi, kinaya, ritifaa na misimu ili kurahisisha uwasilishaji wa maudhui. Utafiti huu unatoa mchango madhubuti katika ukosoaji wa fasihi yoyote ile kwa kuhusisha falsafa za kikale katika kuchambua fasihi za kisasa. Matokeo ya utafiti ni tija kwa wasomi wa fasihi, wahakiki wa masuala ya maadili, wasanii pamoja na Shirika la kudhibiti filamu na muziki nchini Kenya.
English
This research investigated the relevance of Plato’s views on literature. It further highlighted the importance of his opinions on literature in regulating morality in two music pieces due to moral decay. The two pieces which were examined are: Seti by Bahati and Stick by Khaligraph Jones. Despite the firm religious and cultural sensitisation on morality in Kenya, there still exists some modern music which promotes immorality. The two songs stirred emotions and hot debate among many because of the content, yet there is still controversy from the government concerning their censorship. The purpose of this research was to assess if the two songs deserved censorship mainly because of violating moral standards, and to analyse their content using Plato’s views on the role of literature/art. Plato’s Moralist Theory of Art was applied in this research, and its tenets were linked to the objectives. This was qualitative research which applied the descriptive design method in analysing and presenting the collected data. The data was downloaded from the YouTube platform, and thereafter, the visuals and lyrics in the songs were closely analysed. Purposive sampling was employed in selecting the two music pieces that had raised public outcry and concern. The study found that these songs arouse sexual emotions, contain obscene content, promote immorality and corrupt the minds of the audience; therefore, they should be censored. The research makes a significant contribution to literary criticism through the application of classical philosophical views in the analysis of modern literature or texts. The findings are of help to literature scholars, morality and cultural critics, artists and the Kenyan Film and Classification Board.
Keywords: Gengetone, Hip-hop, morality, music, regulation, Sheng
Downloads
Published
How to Cite
Issue
Section
Copyright (c) 2025 James Mwangi

This work is licensed under a Creative Commons Attribution-NonCommercial-ShareAlike 4.0 International License.