Usawiri wa mandhari kibibliotherapia katika hadithi fupi teule za kiswahili
Keywords:
bibliotherapia, hadithi fupi, MandhariAbstract
SWAHILI
Mandhari huwa ni sehemu muhimu katika kazi ya Sanaa. Mtunzi hutumia mandhari kuibua maudhui na sifa za wahusika. Mandhari ni mahali au makazi maalum yaliyojengwa na mtunzi na mnamotukia matukio mbalimbali ya kazi ya fasihi. Makala haya yalilenga kupambanua sifa za kibibliotherapia katika mandhari ya diwani teule za hadithi fupi za Kiswahili. Diwani hizo ni zifuatazo; Mayai Waziri wa Maradhi na Hadithi Nyingine (2004), Damu Nyeusi na Hadithi Nyingine (2007), Kiti cha Moyoni na Hadithi Nyingine (2007) na Tumbo Lisiloshiba na Hadithi Nyingine (2016). Utafiti huu ulifanywa maktabani ambapo data ziliweza kukusanywa kwa kutumia mbinu ya udurusu wa vitabu. Mtafiti alipitia maandishi mbalimbali kutoka katika vitabu teule vya hadithi fupi pamoja na wavuti ili kupata maelezo yaliyotosha kukidhi haja ya Makala haya. Utafiti huu uliongozwa na Nadharia ya Mapatano ya Mwitikio wa Msomaji (NMMM) yake Rosenblatt (1995) ili kumsaidia mtafiti kupambanua sifa za kibibliotherapia katika mandhari. Matokeo ya utafiti huu yalibaini kwamba bibliotherapia hujitokeza katika mandhari yanayosawiriwa katika diwani hizi za hadithi fupi teule.
Downloads
Published
How to Cite
Issue
Section

This work is licensed under a Creative Commons Attribution-NonCommercial-ShareAlike 4.0 International License.