Maudhui kuhusu jinsia katika nyimbo za kampeni za kisiasa katika kaunti ya Bomet, nchini Kenya
Keywords:
Jinsia,Maudhui,nyimbo za kampeni za kisiasaAbstract
SWAHILI
Utafiti huu ulishughulikia namna maudhui ya nyimbo za kampeni za kisiasa huwakilisha jinsia katika Kaunti ya Bomet nchini Kenya. Ulichunguza iwapo nyimbo zilisababisha kuchaguliwa kwa wanaume wengi kuliko wanawake. Lengo mahususi la utafiti huu lilikuwa kufasili namna maudhui ya nyimbo za kampeni za kisiasa huwakilisha jinsia. Utafiti huu uliongozwa na nadharia ya Ubabedume. Huu ni utafiti wa kithamano mkabala wa kifasili. Nyimbo hamsini na mbili za kisiasa zilizorekodiwa katika kanda wakati wa kampeni zilikusanywa. Sampuli ya kimakusudi ilitumika kuteua nyimbo ishirini na mbili za kampeni za kisiasa zilizohusika na jinsia. Deta zilikusanywa kwa usikilizaji wa kanda za nyimbo pamoja na mwongozo wa maswali ya mahojiano. Mbinu ya ufasili wa deta ilitumika katika utafiti huu. Matokeo ya utafiti huu, yalibainisha kwamba nyimbo nyingi za kampeni za kisiasa zilitetea jinsia ya kiume. Nyimbo hizo zilipatia hadhi ya juu jinsia ya kiume kuliko ya kike. Mtafiti anapendekeza kwamba utafiti ufanywe kuhusu namna jinsia ya kike husawirika kupitia maongezi na majadiliano katika mikutano ya kampeni za kisiasa.
ENGLISH
This study addressed how the content of political campaign songs represents gender in Bomet County, Kenya. It investigated whether songs led to the election of more men than women. The specific objective of this study was to interpret how the content of political campaign songs represents gender. This study was guided by Hegemonic Masculinities theory. This is a qualitative study interpretative perspective. Fifty two political songs recorded on tape during the campaign were collected. Purposive sampling was used to select twenty two gender-sensitive political campaign songs. Listening to recorded songs along with an interview guide were used to collect data. Interpretative data analysis was used in this study. The results of this study, identified that many political campaign songs defended the male gender. The songs gave a higher status to men than women. The researcher recommends that research be done on how the female gender is portrayed through conversations and discussions in political campaign rallies.
Keywords: Content, gender, political campaign songs
Downloads
Published
How to Cite
Issue
Section

This work is licensed under a Creative Commons Attribution-NonCommercial-ShareAlike 4.0 International License.