Mbinu za Kimtindo Zinazojenga Utaifa wa Jamii ya Akamba

https://doi.org/10.51317/eajk.v4i1.739

Authors

Keywords:

Arki za utaifa, nyimbo pendwa, utaifa, utaifa wa kijamii, utambulisho

Abstract

Kiswahili

Lengo la utafiti huu lilikuwa kuchunguza jinsi nyimbo pendwa za mwanamuziki Ken wa Maria zinavyoendeleza utaifa wa jamii ya Akamba. Madhumuni ya utafiti huu yalikuwa kuhakiki mbinu za kimtindo zinazotumika kujenga utaifa wa jamii ya Akamba katika nyimbo pendwa teule za Ken wa Maria. Utafiti huu uliongozwa na Nadharia ya Umitindo iliyoasisiwa na Leech pamoja na Short. Nadharia ya Umitindo huchunguza namna msanii wa fasihi hutumia lugha kwa namna ya kipekee ili kumwezesha kuwasilisha ujumbe wake kwa hadhira lengwa. Mihimili ya nadharia hii ndiyo iliyoelekeza utafiti huu wakati wa kukusanya, kuchanganua na kuwasilisha data kwa kuzingatia madhumuni ya utafiti. Muundo wa utafiti huu ni muundo elezi. Utafiti huu ulifanyiwa katika maktaba ili kupata data. Sampuli ya kimakusudi ilitumika ili kupata nyimbo 24 ambazo zilipakuliwa kutoka mtandao wa YouTube na Mdundo.com. Nyimbo hizi zilitafsiriwa katika lugha ya Kiswahili kisha kuchanganuliwa ili kubainisha mbinu za kimtindo alizotumia msanii Ken wa Maria kujenga utaifa wa jamii ya Akamba. Data ilichanganuliwa na matokeo yake kufafanuliwa kwa kutumia mbinu ya kimaelezo. Uwasilishaji wa data ya utafiti ulifanywa kwa njia ya kimaelezo. Utafiti huu ulibaini kwamba kunazo mbinu za kimtindo kama vile jazanda, methali, misemo, chuku, matumizi spesheli ya lugha na misemo iliyotumiwa na msanii kujenga utaifa wa jamii ya Akamba. Utafiti zaidi unaweza kufanywa kuhusiana na mada hii hasa jinsi wasanii wengine kutoka jamii ya Akamba wanavyotalii suala la ujenzi wa utaifa wa jamii.

English

The aim of this study was to investigate how selected popular songs by Ken wa Maria promote nationalism among the Akamba community. The specific objective of the study was to examine literary devices used by Ken wa Maria in his popular music to promote nationalism among the Akamba. This study was guided by the stylistics theory whose proponent is Leech and Short. The stylistics theory holds that language is a significant ingredient in literature. It also argues that the writer uses unique language style to convey the message to the audience. The tenets of this theory were used in collecting and analyzing data in regard to the research objective. The study was descriptive library-based research. The researcher used purposive sampling to identify 24 popular songs by Ken wa Maria which were downloaded from YouTube and Mdundo.com. The songs were transcribed and translated to Kiswahili. An analysis of the stylistic devices used in the songs was conducted. Data was analyzed qualitatively in view of the research objective. This study revealed how the stylistic choices in contextual usage contribute to the promotion of Kamba nationalism among the Akamba. The findings of this research illuminate the significance of popular music in the development of ethno-nationalism. The findings of this study will contribute to the theory of music in oral literature. The study will benefit scholars of oral literature to establish the emerging themes in popular music. It is also bound to benefit constitutional bodies mandated to promote national values and Kenya’s rich culture such as the National Museums of Kenya and the National Cohesion and integration Commission of Kenya in establishing the significance of popular songs in the promotion of national values and conservation of ethnic cultures.

Keywords: Archives of nationalism, identity, nationalism, popular songs, social nationalism

Downloads

Download data is not yet available.

Published

2025-06-12

How to Cite

Munyao, J. K., Nabea, W. K., & Wandera, P. S. (2025). Mbinu za Kimtindo Zinazojenga Utaifa wa Jamii ya Akamba. Eastern Africa Journal of Kiswahili (EAJK), 4(1), 23–38. https://doi.org/10.51317/eajk.v4i1.739

Issue

Section

Articles