Athari ya Uraibu wa Dawa za Kulevya katika Jamii kupitia Nyimbo za Kizazi Kipya Mtandaoni

https://doi.org/10.51317/eajk.v4i1.764

Authors

Keywords:

Athari, mapambano, mihadarati, mtandao, nyimbo za kizazi kipya

Abstract

Kiswahili

Suala la dawa za kulevya ni mojawapo ya masuala ibuka lenye athari kubwa katika jamii huku mtandao ukichangia hali hii. Makala haya yalichunguza madhara yake yalivyosawiriwa katika mapambano dhidi ya mihadarati kupitia nyimbo za kizazi kipya mtandaoni. Kazi hii iliongozwa na Nadharia ya Athari ya Vyombo vya Habari iliyoasisiwa na McLuhan’s (1964). Muundo wa kithamano mkabala wa kiutendaji ulitumika. Mbinu ya ukusanyaji data iliyotumika ni uchanganuzi wa yaliyomo. Mwongozo wa uchanganuzi wa yaliyomo ulitumika kukusanya data mtandaoni. Umma lengwa ulihusisha nyimbo za kizazi kipya na mtandao. Mbinu ya usampulishaji wa kimaksudi ilitumika kuchagua nyimbo za kizazi kipya za Kiswahili, suala la dawa za kulevya na mtandao wa You Tube. Kisha, usampulishaji wa kitabaka ulitumika utabakisha nyimbo kidhima na kwa kurejelea aina tofauti ya mihadarati iliyosawiriwa. Jumla ya nyimbo tano na mtandao mmoja ulilengwa. Kazi hii ililenga kupata data ya kimaelezo iliyowasilishwa kwa kutumia maelezo ya kifafanuzi, mijadala, mifano na dondoo. Matokeo ya kazi hii ni kwamba nyimbo za kizazi kipya ziliangazia athari zake kwa jamii, familia na waraibu wa dawa tofauti za kulevya kama njia mojawapo ya kuhamasisha jamii katika mapambano dhidi ya mihadarati. Makala haya yanapendekeza mitandao mbalimbali tofauti na ule wa YouTube kutafitiwa kwa kurejelea madhara ya mihadarati. Pili, uchunguzi wa athari ya uraibu wa mihadarati kwa kurejelea nyimbo nyinginezo mbali na zile za kizazi kipya. Hatimaye, madhara ya mihadarati pia zitafitiwe katika tanzu nyingine za fasihi pepe kama vile vichekesho, filamu na vipindi vya runinga.

English

Drug and substance abuse are among emerging issues with dire effects on the community, with the internet as a contributor. The fight against drug and substance abuse was portrayed through highlighting its effects on hip hop songs online. The paper was guided by the Mass Media Effect Theory of Marshall McLuhan in 1964. This paper adopted descriptive action design. The method of research was content analysis. The data on hip-hop songs on YouTube were observed using the content analysis tool. The target group was hip hop songs, drugs and substances and the internet. Purposive sampling was used to select Kiswahili hip hop songs, drug and substance abuse and YouTube. Stratified sampling classified songs thematically and in groups based on similar drugs. The paper targeted five songs on YouTube. It aimed at getting descriptive data. The data collected was quantitatively analysed and presented descriptively from extracts of songs and content analysis schedules. The study found that hip hop songs highlighted the effects of drug and substance abuse on the addicts, their families and society at large. There is a need for other internet platforms, such as Facebook and X, among others, to be studied on the effects of drug and substance abuse. Secondly, the effects of drug and substance abuse are to be studied on other songs apart from hip hop songs. Lastly, the effects of drugs and substance abuse should be studied on other genres of oral literature such as comedy, film and television programs.

Keywords: Effects, struggle, drugs, internet, new generation songs

Downloads

Download data is not yet available.

Published

2025-07-21

How to Cite

Ndinyo, S. M., Mohochi, E. S., & Musungu, J. J. (2025). Athari ya Uraibu wa Dawa za Kulevya katika Jamii kupitia Nyimbo za Kizazi Kipya Mtandaoni. Eastern Africa Journal of Kiswahili (EAJK), 4(1), 55–63. https://doi.org/10.51317/eajk.v4i1.764

Issue

Section

Articles

Similar Articles

You may also start an advanced similarity search for this article.