Uchanganuzi wa mielekeo ya wanafunzi kuhusu ufundishaji wa Stadi za Mawasiliano kwa kiswahili katika taasisi za kiufundi za kitaifa nchini Kenya kwa misingi ya michepuo ya masomo

https://doi.org/10.51317/eajk.v3i1.484

Authors

Keywords:

Kiswahili, michepuo, mielekeo, stadi za mawasiliano, wanafunzi wa taasisi za kiufundi

Abstract

SWAHILI

Madhumuni ya utafiti huu yalikuwa ni kuchanganua mielekeo ya wanafunzi wa kozi za sayansi na sanaa kuhusu ufundishaji wa Stadi za Mawasiliano kwa Kiswahili nchini Kenya. Aidha, kuchunguza visababishi vya mielekeo husika kuhusu umuhimu wa matumizi ya Kiswahili kufundisha stadi za mawasiliano. Muundo wa Uchunguzi Kimaelezo ulitumiwa, huku taasisi 5 za kiufundi za kitaifa na sampuli ya wanafunzi 148 wakishirikishwa katika utafiti. Fomula ya Balian (1988) ya uteuzi wa sampuli ilizingatiwa na ukusanyaji wa data ulitumia kitanga cha mielekeo ya hojaji ya Likert kilichokarabatiwa, maswali ya wazi na dodoso. Waaidha, Zanatepe ya Kichanganuzi Data ya Kitakwimu za Sayansi Jamii (SPSS) kilitumika kuchanganua data. Matokeo yalidhihirisha kuwa, asilimia 2.82 ya wanafunzi 142 waliohusishwa katika uchanganuzi walidhihirisha mielekeo hasi, ilhali asilimia 97.18 walionyesha mielekeo chanya kuhusu ufundishaji wa Stadi za Mawasiliano kwa Kiswahili katika taasisi za kiufundi nchini Kenya. Aidha, wanafunzi wa kozi za sanaa walidhihirisha mielekeo chanya ya chini wakilinganishwa na wenzao wa sayansi. Uchanya huu ulitokana na faida ya utoaji wa huduma uwandani kwa wateja wao waliyoiambatanisha na kuridhia Kiswahili kitumike katika ufundishaji wa stadi za mawasiliano. Kwa mkabala huu, wanafunzi wa taasisi husika waliona umuhimu wa mawasiliano kabambe katika utoaji huduma nyanjani. Hivyo, kuanzishwa kwa ufundishaji wa stadi za mawasiliano kwa kutumia Kiswahili sambamba na Kiingereza kungewasaidia kuchonga maarifa yaliyogusia mawasiliano. Matokeo ya utafiti huu ni ya umuhimu kwa Wizara ya Elimu ya Juu, Sayansi na Teknolojia na Taasisi ya Ukuzaji wa Mitaala, Kenya katika utungaji wa sera ya elimu katika taasisi husika.

ENGLISH

This study sought to analyse the attitudes of the students pursuing science and arts courses towards teaching Communication Skills in Kiswahili in Kenyan national polytechnics. Also, to investigate the causes of the attitudes and establish their views on the importance of using Kiswahili in teaching communication skills. A descriptive survey design was used to guide the study. Five Kenyan national polytechnics and a sample of 148 respondents was involved. Balian’s (1988) formula was used to select the sample size. Additionaly, adapted Likert’s scale was used to collect data as well as a questionnaire and open ended questions. Concomitantly, Statistical Package for Social Science (SPSS) was used to analyse the data. The results indicated that 2.82% of the 142 respondents, depicted negative attitude, while 97.18% were mostly positive about being taught Communication Skills in Kiswahili. Students pursuing arts-related courses posted low positive attitudes compared to those pursuing science courses. This positivity seems to have been caused by their realization of the importance of service delivery to their customers in the field, hence the need to use Kiswahili in teaching communication skills in Kenyan technical institutes. In this perspective, the concerned students saw the importance of using effective communication in service delivery in the field. Hence, the use of Kiswahili in teaching communication skills parallel to English would sharpen skills used in communication. The findings of this study are of essence to the Ministry of Higher Education Science and Technology and Kenya Institute of Curriculum Development in developing education policy to the concerned institutions.

Key words: Attitudes, combination, communication skills, Kiswahili, technical institute’s students.

Downloads

Download data is not yet available.

Published

2024-04-01

How to Cite

Kavoi, J. M. (2024). Uchanganuzi wa mielekeo ya wanafunzi kuhusu ufundishaji wa Stadi za Mawasiliano kwa kiswahili katika taasisi za kiufundi za kitaifa nchini Kenya kwa misingi ya michepuo ya masomo. Eastern Africa Journal of Kiswahili (EAJK), 3(1), 8–21. https://doi.org/10.51317/eajk.v3i1.484

Issue

Section

Articles

Similar Articles

1 2 > >> 

You may also start an advanced similarity search for this article.