Kuwezeshwa kwa uchumi kupitia lugha ya kiswahili
Keywords:
Lugha, utamaduni, mawasiliano, maendeleo na uchumiAbstract
SWAHILI
Makala haya yanalenga kuangazia juhudi za nchi za Afrika mashariki na bara la Afrika kutumia Kiswahili kama nyenzo ya mawasiliono miongoni mwao ili kurahisisha mawasiliano na biashara kati ya wananchi wa mataifa haya. Makala haya yametumia data za kimsingi za tafiti za awali katika kufikia hitimisho lake. Lugha nyingine zinazozungumzwa Afrika masharika kando na lugha-mame za wazaliwa wa Afrika mashariki ni, Kiingereza, Kifaransa na Kijerumani. Lugha hizi zilizokuja na mkoloni pia zimepata nafasi kubwa katika jamii ya Afrika kwa ujumla. Siku za hivi karibuni kumeshuhudiwa ongezeko la matumizi ya lugha ya Kichina na mafunzo kutolewa kwa waafrika kwa lugha hii. Hata hivyo, lugha hizi zinaendelezwa kwa mtazamo na imani za waafrika wenyewe. Waafrika wengi wanaamini kuwa, maendeleo na kungeuka kunatokana na lugha hizi za kikoloni. Mitazamo hii ni tata na imelifanya bara la Afrika kuyumba kimaendeleo. Baadhi ya nchi za Afrika zinatumia lugha za kikoloni kama lugha zao rasmi. Hili linalazimisha yeyote anayezuru nchi hizi ajifunze lugha yao ili kuwepo mawasiliano. Hatua zinazochukulia na nchi za Afrika kutafuta lugha ya kutumika katika nchi zote Afrika ni juhudi za kupewa nguvu na kuungwa mkono na kila nchi ya Afrika. maendeleo hutegemea mawasiliano bora na ambayo hufanikishwa na lugha. Kiswahili kuwa lugha yenye asili ya Kiafrika na juhudi hizi za maenezi kutoka kwa nchi za kiafrika basi itakuwa kiunganishi bora cha nchi hizi.
Downloads
Published
How to Cite
Issue
Section

This work is licensed under a Creative Commons Attribution-NonCommercial-ShareAlike 4.0 International License.