Mikakati ya Upole kwenye Hafla za Mazishi: Mifano Kutoka katika Baadhi ya Jamiilugha za Waluhya

https://doi.org/10.51317/eajk.v5i1.1043

Authors

Keywords:

Mikakati ya upole, hafla za mazishi, jamiilugha za Waluhya, umilisi wa kipragmatiki, Nadharia ya Upole

Abstract

Makala hii inachunguza mikakati ya upole inayotumika katika hafla za mazishi miongoni mwa baadhi ya jamiilugha za Waluhya na jinsi inavyochangia katika kukabiliana na matendo ya usemi yanayotishia nyuso za waombolezaji. Utafiti uliongozwa na Nadharia ya Upole ya Leech iliyoboreshwa na Alabdali. Ulitumia mkabala wa kithamano, ambapo data zilikusanywa kupitia uchunzaji shirikishi na mijadala ya makundi. Jumla ya washiriki 40 (wanawake 20 na wanaume 20) walishiriki katika mijadala ya makundi, huku mahatibu 48 (12 kutoka katika kila jamiilugha teule) wakifanyiwa uchunzaji walipokuwa wakihutubu katika hafla za mazishi. Data zilizokusanywa katika mfumo wa hotuba na rekodi za uchunzaji zilisimbwa, zikapangwa katika makundi ya kimaudhui na kuchanganuliwa kwa kuzingatia malengo ya utafiti pamoja na nadharia iliyoongoza utafiti. Matokeo yalionyesha kuwa mahatibu walitumia mikakati mbalimbali ya upole katika kutoa rambirambi, ikiwemo kanuni ya kumsifu msikilizaji, kanuni ya kujitweza, kanuni ya maafikiano, kanuni ya kutojisifu na kanuni ya huruma. Utafiti ulihitimisha kuwa matumizi ya mikakati ya upole huchangia kuendesha hafla za mazishi kwa amani na kudumisha mahusiano mema kati ya waombolezaji. Aidha, wanajamiilugha za Waluhya wanapaswa kuwa na umilisi wa kipragmatiki wa jamiilugha nyingine wanazotagusana nazo ili kuheshimu kanuni za upole. Makala inapendekeza kuwa tafiti zijazo zichunguze udhihirisho wa mikakati ya upole katika jamiilugha nyingine za Waluhya.

Downloads

Download data is not yet available.

Published

2026-07-06

How to Cite

Ongadi, K. O., Wafula, M., & Obuchi, S. (2026). Mikakati ya Upole kwenye Hafla za Mazishi: Mifano Kutoka katika Baadhi ya Jamiilugha za Waluhya. Eastern Africa Journal of Kiswahili (EAJK), 5(1), 79–91. https://doi.org/10.51317/eajk.v5i1.1043

Issue

Section

Articles

Similar Articles

<< < 1 2 3 

You may also start an advanced similarity search for this article.