Nafasi ya Mandhari katika Kukuza Maudhui katika Filamu ya Becky: Uchanganuzi wa Kisemiotiki

Authors

  • Divinah Nyangarisa Catholic University of Eastern Africa, Kenya
  • Rose Mavisi Catholic University of Eastern Africa, Kenya
  • Mary Malenya Kaimosi Friends University College, Kenya https://orcid.org/0000-0003-2091-6131

DOI:

https://doi.org/10.51317/y62syy48

Keywords:

Filamu, ishara, mandhari, maudhui, semiotiki

Abstract

Makala hii ilichanganua namna mandhari inavyofanya kazi kama ishara katika kukuza maudhui katika filamu ya Becky kwa kutumia Nadharia ya Semiotiki. Ingawa tafiti nyingi kuhusu filamu za Kiswahili zimejikita katika lugha, wahusika na ploti, nafasi ya mandhari kama ishara katika kukuza maudhui haijachunguzwa kwa kina katika filamu za mfululizo za Kiswahili nchini Kenya. Utafiti ulitumia muundo wa mchanganyiko wenye mkazo wa ubora, ambapo vipindi 30 kati ya 211 viliteuliwa kwa usampulishaji dhamirifu. Data ilikusanywa kwa kutazama vipindi teule, kunakili mazungumzo yanayohusiana na mandhari na kuchanganua uhusiano kati ya mandhari, vitendo na maudhui. Matokeo yanaonyesha kuwa mandhari ya makazi, kazi, hospitali, polisi, vichakani, makaburini, mandhari ya kidhania na harusi hutumika kama ishara zinazokuza maudhui ya utabaka, kazi, ugonjwa, uhalifu, mauti, tamaa na ndoa. Kwa hiyo, mandhari si usuli wa matukio pekee, bali ni mfumo wa ishara unaoshirikiana na mazungumzo na matendo katika kujenga maana. Makala inapendekeza watayarishaji wa filamu kuzingatia uteuzi na upangaji wa mandhari kama sehemu ya ujenzi wa maudhui, huku tafiti zijazo zikichunguza mwingiliano wa mandhari na mwanga, sauti, muziki, mavazi na upigaji picha. Utafiti huu unaonyesha umuhimu wa mandhari katika kuunganisha fani, maudhui na tajriba ya hadhira katika filamu za mfululizo za Kiswahili.

Downloads

Download data is not yet available.

Published

2026-09-24

Issue

Section

Articles

How to Cite

Nafasi ya Mandhari katika Kukuza Maudhui katika Filamu ya Becky: Uchanganuzi wa Kisemiotiki. (2026). Eastern Africa Journal of Kiswahili (EAJK), 5(1), 181-190. https://doi.org/10.51317/y62syy48

Similar Articles

1-10 of 15

You may also start an advanced similarity search for this article.