Vigezo vya utoaji majina ya asili ya watu katika jamiilugha ya Wagogo
Keywords:
jamiilugha, jina, majina ya asili, vigezo, WagogoAbstract
SWAHILI
Makala haya yamejikita katika kuchunguza vigezo vya utoaji majina ya asili ya watu katika jamiilugha ya Wagogo. Makala haya yameongozwa na swali moja katika kuandaliwa kwake. Swali hilo linauliza: Vigezo gani vinavyotumika katika utoaji wa majina ya asili ya watu katika jamiilugha ya Wagogo? Mbali na kujadili swali hilo muhimu, makala pia yametoa mapendekezo kuhusu njia za kuendeleza matumizi ya majina ya asili ya watu katika jamiilugha husika. Makala haya ni muhimu kwa watu wote yaani wanaotumia majina ya asili ya watu na wasiotumia majina hayo. Data ambayo ilichunguzwa ni sehemu ya data iliyokusanywa kutoka katika wilaya ya Mpwapwa na Chamwino kutoka katika mkoa wa Dodoma nchini Tanzania. Vijiji vya Mima na Gulwe kutoka wilaya ya Mpwapwa na vijiji vya Mvumi Misheni na Handali kutoka wilaya ya Chamwino vimehusishwa. Uchanganuzi na uchambuzi wa data za makala haya umetumia mbinu ya mahojiano na majadiliano ya kundi lengwa katika kukusanya data uwandani na umeongozwa na Nadharia ya Uumbaji ya Sapir- Whorf, (1958) inayosisitiza kwamba lugha ndio msingi wa kuuelewa ulimwengu. Mtu anapojifunza lugha ni kama anatawaliwa na lugha hiyo hata dunia unayoiumba akilini mwako itatokana na dunia ilivyoratibiwa na wasemaji wake. Katika kuchambua na kuwasilisha data, makala haya yametumia mkabala wa kimaelezo. Matokeo ya uchunguzi yamedhihirisha vigezo mbalimbali vya utoaji majina ya asili ya watu katika jamiilugha ya Wagogo. Vigezo hivyo huweza kuwa na mfanano katika mambo fulani na wakati huohuo kunaweza kuwa na upekee unaotafautisha jamiilugha moja na nyingine.
ENGLISH
This article is based on investigating the origin of the names of people in the Gogo language Community. This article has been led by one question in its preparation. The question asks, what criteria are used to give names of people in the Gogo language community? In addition to discussing the key question, the article has suggested ways to develop the use of natural names of people in the relevant community. This article is important to all people who use natural names and those who do not use the names. The investigated data is a part of data collected from the Mpwapwa and Chamwino Districts from the Dodoma Region in Tanzania, Mima and Gulwe from Mpwapwa District, Mvumi Mission and Handali from Chamwino District. This article employed interviews and group discussions to collect data in analysing data. It is dominated by the Sapir-Whorf (1958) Creation Theory, which insists that language is the basis for understanding the world. When you learn a language is, if you governed by the language, even the world you create in your mind will result from the world coordinated by its speakers. In analysing and submitting data, this article has used qualitative methods in defining data. The investigation results have identified the various criteria for the natural names given to the people in the Gogo language community. The criteria may have a variety of factors and, at the same time, may be unique in distinguishing one and the other.
Key terms: community language, Gogo, names, origininal names, parameters
Downloads
Published
How to Cite
Issue
Section

This work is licensed under a Creative Commons Attribution-NonCommercial-ShareAlike 4.0 International License.