Mchango wa Asasi Mbalimbali Katika Kusuluhisha Mizozo ya Ardhi: Tathmini ya Riwaya ya Kovu Moyoni (Habwe, 2014)
DOI:
https://doi.org/10.51317/ghccds82Keywords:
Ardhi, asasi, Baadaukoloni, fasihi ya Kiswahili, mizozo ya ardhiAbstract
Swahili
Makala hii ilichunguza namna asasi mbalimbali zinavyoshiriki katika kuzuia, kudhibiti na kusuluhisha mizozo ya ardhi, pamoja na kujenga upya jamii baada ya migogoro, kama inavyowasilishwa katika riwaya ya Kovu Moyoni (Habwe, 2014). Mizozo ya ardhi nchini Kenya ina mizizi ya kihistoria inayohusishwa na unyakuzi wa ardhi wakati wa ukoloni, mifumo ya umiliki isiyo sawa na matumizi ya ardhi katika ushindani wa kisiasa. Kwa kutumia muundo wa kimaelezo na uchanganuzi wa matini, data ilikusanywa kwa kusoma riwaya kwa kina, kutambua na kuteua dondoo zinazohusu asasi mbalimbali na kuzipanga katika mada za serikali na vyombo vya usalama, mahakama, viongozi wa kisiasa, taasisi za kidini, mashirika yasiyo ya serikali, vyombo vya habari, wapatanishi na mchango wa wananchi. Uchanganuzi uliongozwa na Nadharia ya Baadaukoloni ukizingatia mihimili ya urithi wa ukoloni, mamlaka na unyonyaji, pamoja na upinzani na ukombozi. Matokeo yanaonyesha kuwa asasi hizi zina majukumu tofauti: baadhi huzuia au kudhibiti vurugu, nyingine husaidia waathiriwa na nyingine hushiriki katika upatanishi na ujenzi upya wa jamii. Hata hivyo, uzembe, matumizi mabaya ya mamlaka na maslahi ya kisiasa hudhoofisha juhudi hizo. Makala hii inachangia katika taaluma ya fasihi ya Kiswahili kwa kuonyesha jinsi riwaya inavyowakilisha kwa pamoja uwezo na mipaka ya asasi katika kushughulikia mizozo ya ardhi.
English
This study examined how various institutions participate in preventing, controlling and resolving land conflicts, as well as rebuilding communities in the aftermath of conflicts, as represented in the Kiswahili novel Kovu Moyoni (Habwe, 2014). Land conflicts in Kenya have historical roots in land dispossession during the colonial period, unequal land ownership systems, and the use of land as a tool in political competition. Using a descriptive research design and textual analysis, data were collected through an in-depth reading of the novel, identification and selection of relevant textual excerpts, and their classification into themes relating to government and security agencies, the judiciary, political leaders, religious institutions, non-governmental organisations, the media, mediators and citizens' contributions. The analysis was guided by Postcolonial Theory, focusing on the tenets of colonial legacy, power and exploitation, as well as resistance and liberation. The findings indicate that these institutions perform different roles: some prevent or control violence, others support victims, while others participate in mediation and community reconstruction. However, negligence, abuse of power and political interests undermine these efforts. The study concluded that the government and security agencies can restore security, courts should ensure justice, and non-governmental organisations and religious institutions can support victims. It recommends that government institutions responsible for land strengthen transparency, accountability, and the timely issuance of decisions regarding ownership claims and compensation. The study contributes to Kiswahili literary studies by showing how the novel represents both the potential and limitations of various institutions in addressing land conflicts.
Downloads
Downloads
Published
Issue
Section
License
Copyright (c) 2026 Mary K. Njeru

This work is licensed under a Creative Commons Attribution-NonCommercial-ShareAlike 4.0 International License.



