Urasimishaji wa Kiswahili katika Asasi Tumizi: Mafanikio na Changamoto

https://doi.org/10.51317/eajk.v5i1.1084

Authors

Keywords:

Asasi tumizi, hadhi ya lugha, katiba, lugha rasmi, utekelezaji

Abstract

Makala hii imechunguza hali ya urasimishaji wa Kiswahili katika asasi tumizi nchini Kenya. Inalenga kuangazia mafanikio yaliyopatikana na changamoto zinazokwamisha utekelezaji wa hadhi ya Kiswahili kama lugha rasmi kwa mujibu wa Katiba ya Kenya ya 2010. Utafiti ulifanywa kupitia uchambuzi wa kina wa nyaraka mbalimbali, huku matokeo yakiwa yamewasilishwa kwa njia ya maelezo. Matokeo yanaonyesha kwamba japo hadhi ya Kiswahili imeanza kuamilishwa kutokana na ongezeko la matumizi yake katika sekta za elimu, sheria, utawala, uchumi na afya, mafanikio yaliyopatikana ni madogo. Imebainika kuwa asasi hizi hazijatumia kikamilifu nguvu za kisheria zilizopo katika Katiba ya Kenya (2010) kuhusu hadhi ya Kiswahili kama lugha rasmi. Changamoto za utekelezaji zimetokana pia na mienendo hasi ya watumishi wa umma pamoja na umilishe mdogo wa Kiswahili miongoni mwao. Kwa nyongeza, ukosefu wa sera madhubuti kuhusu utofauti wa lugha nchini Kenya umezuia juhudi za kurasimisha Kiswahili. Hali hii imeongezwa na ukosefu wa tafsiri za nembo na hati za serikali kwa Kiswahili. Makala hii inahitimisha kwamba, ili kuepusha wananchi kuendelea kukosa taarifa na huduma muhimu zinazotolewa na asasi hizi, serikali inahitaji kuchukua hatua za kimkakati na kutoa rasilimali zinazohitajika kwa kuamilisha urasmi wa Kiswahili kwenye asasi husika.

Downloads

Download data is not yet available.

Published

2026-07-17

How to Cite

Odawo, M. A. (2026). Urasimishaji wa Kiswahili katika Asasi Tumizi: Mafanikio na Changamoto. Eastern Africa Journal of Kiswahili (EAJK), 5(1), 92–99. https://doi.org/10.51317/eajk.v5i1.1084

Issue

Section

Articles

Similar Articles

1 2 > >> 

You may also start an advanced similarity search for this article.